Jifunze kuhusu vyuo vya VETA | vocational-education-and-training-authority

Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) ni taasisi ya serikali yenye mamlaka kamili, iliyoanzishwa chini ya Sheria ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Sura ya 82 mnamo mwaka 1994. VETA imepewa jukumu la kutoa, kufadhili na kuratibu elimu na mafunzo ya ufundi stadi nchini Tanzania. Taasisi hii imeanziswa ikiwa na dira inayo sema “Tanzania yenye mafundi wa kutosha na wenye ujuzi stahiki.”

Dhamira kuu ya kuanzishwa kwa taasisi hii chini ya bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania ni kuhakikisha upatikanaji wa ujuzi wa ufundi stadi nchini Tanzania kupitia utoaji na uhamasishaji wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VET) ili kukidhi mahitaji ya soko la ajira kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Misingi ya Misingi ya VETA

  1. Watu Kwanza
    Taasisi imejikita katika kutimiza nia ya wananchi kwa heshima, ustadi na uharaka unaostahili.
  2. Uwezo na Ubunifu
    Imejipanga kukuza ujuzi wa vitendo kwa kukabiliana na changamoto za kiteknolojia na kukidhi mahitaji ya soko la ajira.
  3. Ushirikiano na Uadilifu
    Taasisi imewekwa misingi na kuamini katika kufanya kazi kwa umoja kwa kiwango cha juu cha uadilifu ili kufikia lengo la pamoja.
  4. Uhusiano na Mahitaji
    Veta imesonga mbele katika kuhakikisha kuwa mafunzo na huduma inazotoa ni stahiki na yanayojibu mahitaji halisi ya watu na soko la ajira.

Majukumu ya VETA

i. Kutoa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi

VETA hutoa mafunzo kupitia vyuo vyake vilivyopo katika maeneo mbalimbali nchini. Walimu wa ufundi hufundishwa kupitia chuo maalum cha VETA kinachoitwa Chuo cha Ualimu wa Ufundi cha Morogoro (MVTTC).

ii. Kuwezesha Ufadhili wa Mafunzo ya Ufundi

VETA inaratibu upatikanaji wa fedha kwa ajili ya mafunzo ya ufundi kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Ujuzi (Skills Development Levy – SDL). Chanzo cha mfuko huu ni michango ya waajiri kutoka sekta binafsi inayotokana na sehemu ya mishahara ya wafanyakazi. Vyanzo vingine vya fedha ni miradi ya maendeleo ya serikali, michango ya washirika wa maendeleo, pamoja na mapato ya ndani kama ada za mafunzo na shughuli za uzalishaji mali.

iii. Kuhamasisha Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi

VETA ina jukumu la kuelimisha na kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa elimu na mafunzo ya ufundi. VETA inaamini kuwa wananchi wanaweza kuunga mkono elimu ya ufundi endapo utapewa taarifa sahihi kuhusu malengo na shughuli zake.
Uhamasishaji huu hufanyika kwa kushirikisha wadau mbalimbali kama serikali, wazazi, waajiri, wafanyakazi, wahisani, wanafunzi wa sasa na watarajiwa, wakufunzi, wahitimu wa VETA, wabunge, vyama vya wafanyakazi, mashirika yasiyo ya kiserikali, na vyombo vya habari.

VETA hutumia njia mbalimbali za mawasiliano kama vile vyombo vya habari, matangazo, maadhimisho ya Wiki ya VETA, maonyesho ya biashara na kazi, machapisho ya jarida, ripoti za mwaka, vipeperushi, katalogi za mafunzo, tovuti rasmi, na nyenzo nyingine za uhamasishaji.

Utoaji wa Mafunzo

Mafunzo ya VETA yamepangwa katika sekta kumi na tatu (13) za taaluma ambazo ni:

  • Uhandisi wa Mitambo (mechanical engineering)
  • Uhandisi wa Umeme (electrical engineering)
  • Ujenzi na Uhandisi wa Majengo (civil engineering
  • Magari na Usafiri (automotive)
  • Huduma za Biashara na Uendeshaji (Commercial Services and Business Support)
  • Ushonaji na Nguo (Clothing and Textile)
  • Uchimbaji Madini (mining)
  • Uchapaji (printing)
  • Urembo na Utengenezaji wa Nywele (Cosmetology)
  • Kilimo na Uchakataji wa Chakula (Agriculture and Food Processing)
  • Ukarimu, Utalii na Uwakala wa Usafiri (Hospitality, Tourism and Travel Agency)
  • Sanaa za Uchoraji, Muziki na Maonesho (Fine and Performing Arts)

Muundo wa Kiutawala

VETA inasimamiwa na Bodi ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VET Board).
Wakati wa kuanzishwa kwa VETA, Bodi hii iliundwa ili kusimamia mfumo mzima wa elimu ya ufundi nchini. Ni chombo cha utungaji wa sera chenye jukumu la kuhakikisha utekelezaji wa majukumu na usimamizi wa shughuli zote za mamlaka.

Bodi ya VET inaundwa na wajumbe kumi na mmoja (11) ambapo Mwenyekiti huteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na wajumbe wengine kumi huteuliwa na Waziri mwenye dhamana ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi.

Wajumbe hao kumi huteuliwa kwa mapendekezo yafuatayo:
i. Wajumbe wawili kutoka mashirika yanayowakilisha waajiri;
ii. Wajumbe wawili kutoka vyama vya wafanyakazi (kuwakilisha wafanyakazi);
iii. Wajumbe watatu kutoka wizara zinazohusika na viwanda, elimu na ajira;
iv. Wajumbe watatu kutoka mashirika yasiyo ya kiserikali yanayosimamia taasisi za mafunzo ya ufundi.

Wajumbe wote wanaoteuliwa lazima wawe watu wenye sifa na uwezo wa kuchangia maendeleo ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi nchini.
Kipindi cha uongozi cha wajumbe wa bodi ni miaka mitatu (3), na baada ya kumalizika wanaweza kuteuliwa tena.

VETA administration

VETA administration

Leave your thoughts