Dunia ya magari imejaa ubunifu, teknolojia ya hali ya juu, na hadhi inayovutia. Magari hayaishii tu kuwa chombo cha kurahisisha usafiri bali wabunifu wamizidi kwenda mbali na kuunda magari yanayo simama kama alama ya kuwakilisha ukwasi wa mtu, ubunifu, kiwakilishi cha utaifa, ubora wa watengenezaji pamoja na hadhi ya kijamii. Kuna magari mengi sana na yenye sifa za kipekee lakini hapa nimekuwekea magari 8 ya kifahari duniani
8. Lamborghini Veneno
Nchi iliyotengenezwa: Gari imetengenezwa nchini Italia na kampuni ya Automobili Lamborghini S.p.A
Sifa za gari: Injini aina ya V12, Uwezo wa kutoka speed 0 had 100km/hr ndani ya sekunde 2.9, Nje imetengenezwa na material ya kabon(carbon fibers),
Top speed: 355 km/h
Idadi ya gari: zimetengenezwa gari 13 tu duniani moja ya wamiliki wa gari hizo ni familia ya kifalme ya saudia, muwekezaji mashuhuri wa jimbo la florida Kris Singh pamoja na Antoinne Dominic
Utaratibu wa kununua: Kwa sasa njia pekee ya kununua ni kuwasiliana na wamiliki walio zinunua tayari ili waweze kukuuzia kwa sababu lamborghini hawata tengeneza tena gari ya aina hiyo(Limited edition)
Bei: $4.5 milioni (Tsh 11,016,449,993) zaidi ya bilion 11 za kitanzania

7. Koenigsegg CCXR Trevita
Nchi iliyotengenezwa: Gari imetengenezwa nchini Uswidi(sweeden) na kampuni ya Koenigsegg Automotive AB
Sifa za gari: Inayo injini ya V8 twin-supercharged yenye uwezo mkubwa sana, Ndani yake kuna viti vya ngozi, mfumo wa sauti wa hali ya juu, Kwa nje imeundwa na kabon(carbon fiber) yenye mng’ao wa almasi moja ya teknolojia adimu na ghali sana duniani, Uwezo wa kutoka speed 0 had 100km/hr ndani ya sekunde 3.1
Top speed: 410 km/h (255 mph)
Idadi ya gari: Gari hizi zilitengenezwa mbili tu duniani na wamiliki wake ni mcheza ndondi mashuhuri duniani kutoka Marekani Floyd Mayweather na kampuni ya uuzaji wa magari maarufu nchini uswizi ambapo baadae iliuzwa kwa kampuni nyingine ya uuzaji magari Dubai
Utaratibu wa kununua: Awali gari hizi ziliuzwa kwa kibali maalumu ambacho mmiliki alitakiwa kukiomba kutoka kampuni ya Koenigsegg Automotive AB bila kusahau gharama za kuomba kibali ni ($50,000 non refundable) swana na Tsh. 122404999 pesa ambayo haitarudishwa hata kama ukikataliwa maombi yako. Lakini kwa sasa hakuna namna ya kupata hilo gari isipokuwa kuwafata wamiliki ili wakuuzie.
Bei: $4.8 milioni (takribani TSh bilioni 12.5)

Koenigsegg CCXR Trevita
6. Mercedes-Maybach Exelero
Nchi iliyotengenezwa: Ujerumani (Germany) Imetengenezwa na kampuni ya Maybach, kwa ushirikiano na Fulda Tires upande wa matairi
Sifa za gari: V12 Twin-Turbocharged, Uwezo wa kutoka speed 0–100 km/h kwa Sekunde 4.4, viti vyake ni vya ngozi na sehem kubwa upande w nje imetumia mbao za kisasa
Top speed: 351 km/h
Idadi ya gari: Kwakuwa lilikuwa ni kwa ajili ya majaribio gari hili lipo moja tu duniani. Kampuni shiriki katika kutengeneza Fulda ndio mmiliki alie linunua. Baadae liliuzwa kwa mwanamuziki mashuhuri na mwenye ukwasi nchini marekani Brayan Wilson(Birdman) ambapo kuna taarifa zisizo rasmi kuwa aliliuza kwa moja ya makampuni ya kuuza magari nchini kwake
Utaratibu wa kununua: Hakuna utaratibu wa kupata likiwa jipya kwa sasa njia pekee ni kumfata mmiliki na kuomba mauziano.
Bei: Takribani $8 milioni (sawa na TSh bilioni 21)

Mercedes-Maybach Exelero
5. Bugatti Centodieci
Nchi iliyotengenezwa: Gari imetenegenezwa nchini Ufaransa (France) na kampuni ya Bugatti Automobiles S.A.S.
Sifa za gari: Injini W16 8.0-liter Quad-Turbo, Uwezo wa kutoka speed 0–100 km/h kwa Sekunde 2.4, kulinganisha na matoleo mengine ya bugati hii imeundwa ikiwa na uzito mdogo zaidi, ngozi upande wa ndani ni ya ubora wa hali ya juu pamoja na teknolijia ya kisasa
Top speed: 380 km/h (236 mph)
Idadi ya gari: Gari hizi zilitengenezwa 10 tu duniani na kati ya hao wote ni mmiliki mmoja tu ambae ni mchezaji wa kandanda mwenye ukwasi kuliko wote Cristiano Ronaldo dos santos ndie tarifa zake zilitoka lakini wengine walisisitiza faragha katika kampuni hiyo kabla ya kununua.
Utaratibu wa kununua: Gari hizi hazikuuzwa kila mtu isipokuwa wateja wa kudumu wa bugati na hivyo basi hakukuwa na nafasi ya umiliki kwa watu wengine. Kuzipata kwa sasa unatakiwa uwasiliane na wamiliki wa awali ili waweze kukuuzia
Bei: $9 milioni (takribani TSh bilioni 23.6)

Bugatti Centodieci
4. Rolls-Royce Sweptail
Nchi iliyotengenezwa: Gari hii imetengenezwa mwaka 2017 Uingereza (United Kingdom) chini ya kampuni maarufu ya magari ya kifahari Rolls-Royce Motor Cars Limited, ambayo ni tawi la kampuni.
Sifa za gari: uwezo wa injini 6.75-litre V12 petrol engine, Uwezo wa kutoka speed 0–100 km/h kwa Sekunde 5.6. Gari hii imetengenezwa kwa mikono kwa sehemu kubwa tofauti na gari nyingine hutumia maroboti. Gari hii imetengenezwa kwa kufananisha muonekano na boat za kifahari(yatch). Upande wa juu ndani ya gari(roof) gari imewekwa kioo kirefu cha panoramic glass roof kinachoruhusu mwanga wa asili kuingia. upande wa viti imeboreshwa kwa ngozi yenye ubora wa hali ya juu. Injinia alie tengeneza gari hili alichora kwa mkono mwanzo mwisho
Top speed: 250 km/h (155 mph)
Idadi ya gari: gari hili lilitengenezwa moja tu na mmiliki hakuwahi kutangazwa hadharani na kampuni kwa ajili ya kulinda faragha.
Utaratibu wa kununua: Gari hii haikuwahi kuuzwa kabisa wala kuwepo katika minada. Njia pekee ya kulinunua ni kuomba mmiliki akuuzie au alipige mnada.
Bei: $13 milioni (takribani TSh bilioni 34)

Rolls-Royce Sweptail
3. Pagani Zonda HP Barchetta
Nchi iliyotengenezwa: Gari imetengenezwa nchini Italia (Italy) chini ya kampuni ya magari ya kifahari Pagani Automobili S.p.A, mwaka 2017.
Sifa za: injini ya 7.3-litre Naturally Aspirated V12, yenye uwezo wa kutoka speed 0-100km/h ndani ya sekunde 2.9 tu. Upande wa nje wa gari imetumika kabon(carbon fiber) na titanium kuweza kupata uimara, wepesi na muonekano ulio bora. Gari ni kibanda wazi(open top). Limeboreshwa uzito takribani kufikia kilogram 1250 tu.
Top speed: 355 km/h (220 mph)
Idadi ya gari: Gari zilitengnezwa 3 tu ambapo moja analitumia mmiliki wa kampuni mwenyewe, la pili lilinunuliwa na tajiri kutoka japani lakini hakutaka jina lake liwekwe hadharani. Mwisho ni mfanyabiashara kutoka uingereza ambae pia jina lake halikuwekwa hadharani moja kwa moja
Utaratibu wa kununua: gari hii haikuwahi kuuzwa hadharani ilitengenzwa kwa heshima kumuenzi muanzilishi Horacio Pagani. kwa wamiliki walio nazo sasa hakujawahi kuwa na taarifa rasmi ya kuuza hivyo zipo katika maonesho tu
Bei: $17.5 milioni (takribani TSh bilioni 45.5)

Pagani Zonda HP Barchetta
2. Bugatti La Voiture Noire
Nchi iliyotengenezwa: Imetengenezwa nchini Ufaransa (France)na kampuni ya gari za kifahari Bugatti Automobiles S.A.S mwaka 20219
Sifa za gari: Uwezo wake wa injini ni 8.0-litre W16 Quad-Turbocharged yenye uwezo wa kutoka speed 0-100km/h ndani ya sekunde 2.4 tu. Limetengenezwa kwa carbon nyeusi safi(black carbon fiber) kama jina lake lilivyo kwa lugha ya kifaransa likimaanisha rangi nyeusi. kama ilivyo desturi ya kampuni ya rolls royce gari hii nayo imetengenezwa kwa mikono ikitumia chuma chenye bei ghali upande wa nje, ngozi ya thamani kwenye viti na technolojia y ahali ya juu.
Top speed: 420 km/h (261 mph)
Idadi ya gari: gari hii ilitengenezwa moja tu kwa aina yake na mmiliki hakuwahi kuwekwa hadharani na kampuni hiyo japokuwa kulikuwa na taarifa zisizo rasmi kuwa marehemu Ferdinand Piëch alikuwa mmiliki wa volkswagen group ndie alie nunua. Pia Ronaldo aliwah kuhusishwa na umiliki wa gari hiyo lakini msemaji wake alitoka hadharani kupinga hilo.
Utaratibu wa kununua: Gari hili licha ya kuchukua miaka 2 na miezi sita kulitengeneza halipatikani sokoni na hata mmiliki hajulikani hivyo huwezi kulipata mpaka litakapo wekwa kwenye mnada
Bei: $18.7 milioni (takribani TSh bilioni 49)

Bugatti La Voiture Noire
1. Rolls-Royce Boat Tail
Nchi iliyotengenezwa: Gari imetengenezwa nchini Uingereza (United Kingdom) na kampuni maarufu ya kifahari Rolls-Royce Motor Cars Limited mnamo mwaka 2021.
Sifa za gari: Gari imeundwa na injini ya kipekee aina ya 6.75-litre V12 Twin-Turbocharged yenye uwezo wa kutoka speed 0-100km/h ndani ya sekunde 5. Kama ilivyo kwa magari mengine ya kampuni hiyo, hili nalo limeundwa kwa mikono na likiwekewa aluminium kwa wingi ikiwa ni mbadala wa chuma. Jina la gari limepatikana kwa kufananisha boti za kisasa upande wa nyuma(boat tail). Ina sehemu ya nyuma inayofunguka automatiki huku ikiwa na friji, glasi za champagne, sahani na vibao vya chakula.
Top speed: 250 km/h (155 mph)
Idadi ya gari: Magari haya yametengenezwa matatu (3) tu. Mmoja wao ni wanandoa maarufu na waimbaji nchini marekani Jay-Z & Beyoncé (Marekani). La pili lilinunuliwa na tajiri wa kutoka uswisi. Wa mwisho ni mmiliki binafsi kutoka Italia ambae ndie alie shirikiana na kampuni katika ubunifu huu.
Utaratibu wa kununua: Gari hii haiuzwi kabisa wala wamiliki wake hawajawahi kulihusisha katika minada
Bei: $28 milioni (takribani TSh bilioni 73)

Rolls-Royce Boat Tail