Chuo Cha Usafirishaji (NIT) ni Taasisi ya Umma ya Elimu ya Juu iliyoanzishwa chini ya Sheria ya NIT Sura ya 187, ikiwa na jukumu kuu la kutoa elimu na mafunzo, kufanya tafiti pamoja na kutoa ushauri elekezi katika nyanja za Usafirishaji, Usimamizi na Teknolojia ya Uchukuzi. Taasisi hii ipo chini ya Wizara ya Uchukuzi.
Makao yake makuu yapo upande wa magharibi mwa Jiji la Dar es Salaam, katika eneo la viwanda vidogo vya Ubungo, barabara ya Mabibo. NIT imepewa kibali na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) kutoa mafunzo ya msingi katika ngazi za Astashahada, Stashahada, Shahada na Shahada ya Uzamili (NTA ngazi ya 4 hadi 9).
Taasisi ina jumla ya watumishi 421, ambapo 270 ni wahadhiri wa muda wote. Kati yao, wamo Maprofesa 2 pamoja na Wakufunzi Wakuu, Wahadhiri, Wasaidizi wa Wahadhiri, Wakufunzi na Wataalam wa maabara. Pia kuna watumishi wa kada za utawala wapatao 151.
Ngazi za Elimu Zinazotolewa na Chuo Cha NIT
- Elimu ya Masuala ya Ndege (Aviation),
- Masuala ya Bahari na Mafuta (Maritime and Petroleum Technology),
- Uhandisi na Teknolojia ya Usafiri,
- Usafirishaji na Biashara (Logistics and Business Studies),
- Faculty ya Tehama na Masomo ya Ufundi (Informatics and Technical Studies).
Mambo Ya Msingi Na Yanayo Pewa Kipaumbele Chuo Cha NIT
Malezi – Tunajitahidi kulea, kukuza na kuandaa wataalam katika masuala ya usafiri na fani zinazohusiana nayo.
Uadilifu – Tunatoa huduma bora kwa weledi, tukizingatia kiwango cha juu cha ukweli, uaminifu na kutokuwa na upendeleo, huku tukifuata maadili ya kitaaluma.
Ushirikiano – Tunafanya kazi kama familia ili kutimiza malengo ya Taasisi na kukidhi matarajio ya wadau wake.
Utofauti wa Kitamaduni – Tunahakikisha mazingira rafiki na jumuishi kwa watu wa asili, mitazamo, tamaduni na mtindo tofauti wa kufikiri.
Uwajibikaji – Tunafuata misingi bora ya utawala kwa kutoa huduma zetu kwa uwazi, huku tukiwa tayari kuwajibika kikamilifu kwa matendo na maamuzi yetu.
Ubunifu – Tunathamini na kuhamasisha fikra mpya, ubunifu na uvumbuzi.
Malengo ya kuanzishwa Chuo Cha Usimamizi Wa Fedha
- Kutoa mazingira na miundombinu ya kusomea na kujifunzia kanuni, taratibu na mbinu za uendeshaji wa usafirishaji, usambazaji wa bidhaa pamoja na masomo mengine yanayohusiana, kulingana na maamuzi ya Baraza kadri muda unavyokwenda.
- Kufanya mafunzo katika programu mbalimbali na masomo mengine yanayofanana, kama Baraza litakavyoamua mara kwa mara.
- Kujihusisha na utafiti kuhusu changamoto za uendeshaji, upangaji na mahitaji ya mafunzo katika maeneo mbalimbali ya sekta ya usafiri, pamoja na kutathmini matokeo ya mafunzo yanayotolewa na Taasisi.
- Kutoa huduma za ushauri (ushauri elekezi) kwa Serikali, mashirika ya umma na taasisi au watu binafsi pale inapohitajika.
- Kudhamini, kuratibu na kutoa huduma na miundombinu kwa ajili ya mikutano na semina.
- Kuanzisha idara mbalimbali ndani ya Taasisi kwa ajili ya kuratibu na kusimamia shughuli zake.
- Kufanya mitihani ya kitaaluma na kutunuku shahada za uzamili wa kitaaluma, shahada za kawaida, stashahada, vyeti na tuzo nyingine zinazotolewa na Taasisi.
- Kutekeleza majukumu na shughuli zote ambazo kwa maoni ya Baraza ni muhimu au zinazohitajika ili kuhakikisha Taasisi inafanya kazi zake ipasavyo na kwa ufanisi.
- Kupanga na kuratibu uchapishaji na usambazaji wa nyaraka na maandishi yanayohusiana na kazi na shughuli za Taasisi.
- Kuanzisha na kukuza mahusiano ya karibu na taasisi nyingine za elimu ya juu.