Taasisi ya usimamizi wa Fedha | IFM

Tangu kuanzishwa kwake mwaka 1972, Taasisi ya Usimamizi wa Fedha (IFM) imekuwa taasisi ya kwanza na kongwe ya elimu ya juu ya kifedha nchini Tanzania. Kwa muda wote, IFM imejikita katika kutoa elimu bora, kufanya tafiti zenye ubora wa kimataifa, na kutoa ushauri wa kitaalamu. Hadi sasa, taasisi hii ina takribani wanafunzi 15,000 wanaosoma katika ngazi za shahada ya kwanza na za uzamili.

Chuo cha IFM, wanafunzi hupewa motisha na kuhimizwa juu ya kuchunguza masuala muhimu ya karne ya 21 katika nyanja za usimamizi wa fedha, bima, ulinzi wa kijamii, na teknolojia ya habari. IFM inajivunia kutoa mazingira bora ya kujifunzia, ndani na nje ya darasa, yanayomwezesha mwanafunzi kukuza ujuzi na ubunifu.

Taasisi ina elimu katika ngazi tano zinazotoa vyeti, stashahada, shahada, stashahada za uzamili, na shahada za uzamili (masters). Aidha, IFM hutoa mafunzo ya muda mfupi mara kwa mara ili kukidhi mahitaji maalum ya soko la ajira. Hadi sasa, taasisi hii ina zaidi ya wahitimu 50,000 waliotoka katika nyanja mbalimbali.

Dira (Vision) Ya IFM

Kuwa taasisi ya elimu ya juu inayotambulika duniani kwa ubora na inayojibu mahitaji ya maendeleo ya kimataifa kupitia utoaji wa maarifa na umahiri katika usimamizi wa fedha na fani zinazohusiana.

Dhamira (Mission) Ya IFM

Kutoa mafunzo bora ya kitaaluma na kitaalamu yanayokuza ubunifu na fikra bunifu kupitia mafunzo jumuishi, utafiti na ushauri wa kitaalamu katika masuala ya fedha na taaluma zinazohusiana.

Taasisi itaendelea kuwa nguvu ya mabadiliko katika maendeleo ya sekta za umma na binafsi kwa kutoa elimu bora, mafunzo yanayoendana na mahitaji ya soko, pamoja na huduma za utafiti na ushauri wa kitaalamu.

Vitu vya muhimu vinavyo zingatiwa (Core Values)

Kwa kuzingatia Dira yake, Dhamira yake, na falsafa inayoiongoza, IFM imejikita katika kufuata thamani kuu nane (8) zinazofupishwa kwa neno ATTITUDE, kama ifuatavyo:

  1. UBORA NA UFANISI (EXCELLENCE AND EFFICIENCY)
    • Kutoa huduma bora, za haraka na zenye viwango vya juu kwa wadau wote wa taasisi wakati wote.
  2. UJUMUISHO NA USAWA WA KIJINSIA (DIVERSITY & GENDER EQUITY)
    • Kuthamini utofauti na kuhakikisha usawa wa kijinsia katika shughuli zote za taasisi ili kuimarisha ushirikiano na kutumia vyema rasilimali watu zilizopo.
  3. UADILIFU NA UBUNIFU (INTEGRITY AND INNOVATIVENESS)
    • Kuonesha uaminifu, uadilifu na uaminika katika kazi zote, pamoja na kukumbatia teknolojia mpya na mbinu bunifu katika utendaji kazi.
  4. USHIRIKIANO (TEAMWORK)
    • Kukuza utamaduni wa kufanya kazi kwa pamoja kwa moyo wa huruma na mshikamano ili kuongeza ufanisi katika kazi.
  5. UMOJA (UNITY)
    • Kuhimiza umoja ili kuimarisha ushirikiano na mafanikio ya pamoja.
  6. UWAZI NA HAKI (TRANSPARENCY AND FAIRNESS)
    • Kufanya kazi kwa uwazi, kuwa tayari kukaguliwa na umma, na kutumia kanuni na viwango sawa kwa wote.
  7. UWAWAJIBIKAJI (ACCOUNTABILITY)
    • Kuwa na uwajibikaji wa hali ya juu kwa wadau na jamii kwa ujumla, huku tukionesha kujituma katika kuhudumia wateja kwa viwango vya juu vya kuridhisha.
  8. KUAMINIKA (TRUST)
    • Kujenga na kudumisha uaminifu katika kila mahusiano na wateja pamoja na wadau wengine wa taasisi.
Taasisi ya usimamizi wa Fedha

Taasisi ya usimamizi wa Fedha

Leave your thoughts